Maafisa wa ghana wamewakamata raia wawili wa uingereza kwa kujaribu kusafirisha kilo 166 za dawa za kulevya

Raia wawili wa Uingereza wamekamatwa jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kotoko nchini Ghana kwa tuhuma za kujaribu kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine kwenda jijini London.


Watu hao waliokuwa wakijiandaa kusafiri na Ndege ya Shirika la Ndege la Uingereza British Airways, walikamatwa na kilo 166 za dawa za kulevya zenye thamani ya dola za Kimarekani Milioni 6.48.

Dawa hizo zilikuwa zimefichwa ndani ya masanduku sita tofauti.

Kwa muda mrefu sasa Ghana imekuwa ni kituo maarufu cha kupitisha dawa za kulevya kuelekea Ulaya na Marekani kinyume na sheria,hali iliyopelekea kuimarishwa kwa ulinzi.

Share: