Kenya: idadi ya waliofariki kwa mafuriko yaongezeka huku miili ya watu ikiendelea kupatikana

Zaidi ya familia 20,000 zimetoroka makazi yao katika kaunti tatu zilizoathirika za Mombasa, Kilifi, Kwale na Tana River

Miili ya wafanyikazi wawili wa shirika la ushuru nchini Kenya ambao walikuwa wamesombwa na mafuriko walipokuwa wakiendesha gari katika eneo la pwani siku ya Ijumaa ilipatikana siku ya Jumapili.

kikosi cha Walinzi wa Pwani ya Kenya pia waliuchukua mwili wa mwanamume aliyesombwa na maji alipokuwa akiendesha pikipiki yake.

Mamlaka siku ya Jumamosi ilisema kuwa watu 10 wamethibitishwa kufariki katika ufuo huo kufuatia siku tatu za mvua kubwa isiyoisha na mafuriko.

Zaidi ya familia 20,000 zimetoroka makazi yao katika kaunti tatu zilizoathirika za Mombasa, Kilifi, Kwale na Tana River, kamishna wa polisi wa eneo la Pwani Rhoda Onyancha alisema Jumamosi.

Kwa ujumla, makumi ya watu wamefariki na maelfu kuhama makazi yao kote nchini humo tangu mwanzoni mwa Novemba baada ya kuanza kwa mvua kubwa na mafuriko yaliyosababishwa na hali ya hewa ya El Niño.

Mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko imesababisha vifo vya makumi ya wengine katika nchi jirani, zikiwemo Somalia na Ethiopia.

Share: