Katibu wa CCM wilaya ya Kilolo auwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana

Aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Kilolo Mkoani Iringa Christina Kibiki Usiku wa Kuamkia leo ameuawa kwa kupigwa Risasi na watu ambao bado mpaka sasa hawajajulikana.

Hata hivyo St Bongo Tv tulifika nyumbani Nyumbani ulipo msiba Huo ambapo inadaiwa watu wasiojulikana walifanya uvamizi huo usiku wa kuamkia leo katika kitongoji cha Banawanu kijiji cha Ugwachanya mkoani Iringa Nyumbani kwake alipokuwa akiishi 



Vilevile St Bongo Tv imemtafuta kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Allan Bukumbi ambapo amesema tukio hilo la mauaji bado wanalichunguza lakini marehemu alifariki akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Tosamaganga baada ya shambulio hilo la kupigwa risasi eneo la kifuani na kitu kizito kichwani na watu bado ambao hawajafahamika

Share: