Katavi: wafanyabiashara wa soko la majimoto kumuondoa afisa mfawidhi wa kituo cha majimoto

Wafanyabiashara wa Soko la Majimoto lililopo Halmashauri ya Mpimbwe wameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa kumuondoa Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Majimoto, Fraseck Mwakalenga, kwa madai ya kukusanya kodi kiholela na kutoa Lugha chafu na ya kukera

Wanadai wanakadiriwa kiwango cha juu ambacho hakiendani na Biashara zao na kudai hana Heshima kwa Wafanyabiashara jambo ambalo limesababisha baadhi yao kufunga Biashara

Akijibu malalamiko hayo, Meneja wa TRA Mkoa, Nicholaus Migera amesema “Nimechukua maoni, tunayafanyia Kazi lakini siwezi kuondoka naye kwa kuwa nitalazimika kuendelea kumlipa ikiwa hafanyi kazi hadi barua itakapotoka kama anahamishwa au anachukuliwa hatua nyingine, hivyo tuwe na subira tutapata majibu.”

Share: