Johannesburg: miili ya watanzania 3 waliofariki dunia kwa ajali ya moto agosti 31, 2023 itarejeshwa nchini

Ubalozi wa Tanzania, nchini Afrika Kusini umesema miili ya Watanzania 3 waliofariki dunia kwa ajali ya moto Agosti 31, 2023 huko Jijini Johannesburg itarejeshwa Nchini, Januari 24, 2024 baada ya kutambuliwa.

Taarifa ya Ubalozi imeeleza mwili wa Said Kisarazo na Mohamed Kisarazo itaondoka Afrika Kusini Januari 24, 2024 Usiku huku mwili wa Mohamed Amir utaondoka Afrika Kusini Januari 25 saa 2:30 asubuhi na kuwasili Tanzania saa saba mchana.

Mnamo Agosti 31, 2023, moto mkubwa ulizuka katika ghorofa la #Usindiso, uliogharimu maisha ya watu 77 huku ukiwaacha wengi na Majeraha, ambapo hadi sasa Mwanaume mmoja (29) anashikiliwa kwa kukiri kuwasha moto huo huku Polisi ikisema anatarajiwa kufikishwa Mahakamani anapokabiliwa na Mashtaka 120 ya Jaribio la Mauaji.

Share: