Jeshi la polisi dar es salaam linachunguza tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa miaka saba kwenye msitu wa Jeshi

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linachunguza tukio la kuuawa kwa Mtoto wa umri wa Miaka 7, Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kibonde Maji B, Mbagala na mwili wake kukutwa kwenye Msitu wa Jeshi karibu na Shule aliyokuwa anasoma mnamo Machi 13, 2024. 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, SACP Muliro J. Muliro amesema Mtoto huyo kabla ya kupotea aliondoka nyumbani kwao na Mtoto mwenzake Machi 12, 2024, Saa 11:30 Jioni. 

Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Polisi Kilwa Road kwa uchunguzi zaidi wakati zoezi la kutafuta Mtuhumiwa au Watuhumiwa likiendelea. 

Share: