Jela miaka 20 kwa kukutwa na bangi

Mwanamke mmoja Mkazi wa Kisiwa cha Maisome kilichipo Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, Maisala Ramadhani (25) amejikuta anaangua kilio Mahakamani baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka 20 baada kukiri kosa la kukutwa na bangi kilo 10 nyumbani kwake. 

Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 121/2023, imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Sengerema, Evod Kisoka ambapo awali akisoma maelezo mbele ya Hakimu, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Morice Mtoi amesema Mshtakiwa alikamatwa October 9, 2023, na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya ya Sengerema, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Titho Mohe.

Mshtakiwa alikamatwa na Askari huyo katika Kisiwa cha Maisome kambi ya Wavuvi ya Migongo akiwa na bangi kilogramu 10 kwenye nyumba yake ya kuishi.

Share: