Jela miaka 10 unyanyasaji wa kingono

Mwalimu wa shule binafsi ya Kibaptisti huko Wisconsin Marekani amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la unyanyasaji wa kingono wa mara kwa mara kwa mvulana wa miaka 14.

Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 75, Anne Nelson-Koch, pia alipewa kifungo cha uangalizi (probation) miaka 15. Hapo awali alikabiliwa na zaidi ya miaka 600 jela, lakini tabia yake ilizua mzozo na akapunguziwa kifungo mahakamani.

Mnamo Aprili 2022, Nelson-Koch alishtakiwa na polisi kwa kumlazimisha mwanafunzi wake wa kiume, ambaye alikuwa na umri wa miaka 14 wakati wa shambulio hilo, kushiriki ngono wakati wa saa za shule katika mwaka wa masomo wa 2016-2017.

Share: