India: mwanaume mmoja atishia kuua abiria ndani ya ndege

Mwanaume mmoja alishushwa kwenye ndege nchini India leo baada ya kuvua nguo, kujaribu kuchoma blanketi kwa moto na kutishia kuua abiria wakati wa ugomvi na mkewe.

Raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 53, ambaye jina lake halijatajwa, aliburutwa nje ya ndege na wanajeshi huko New Delhi, India, baada ya ndege kulazimika kubadili njia yake iliyopangwa kutoka Munich kuelekea Bangkok, China asubuhi na mapema siku ya Jumatano.

Mashahidi waliokuwemo kwenye Ndege ya Lufthansa walisema kwamba tukio hilo lilitokea ghafla baada ya mke wa mwanaume huyo kumwambia mhudumu wa ndege kwamba alihisi 'anatishiwa' na mumewe na kuomba wafanye kitu kama masaa machache tu baada ya kuanza kwa safari.

Katika mkurupuko wa ajabu wa hasira, abiria huyo alianza kutupa chakula, alijaribu kuchoma blanketi kwa kutumia kibiriti, alivunja simu yake mwenyewe na kuvua nguo zake, mashahidi walisema. 

'Nitawaua wote!' aliripotiwa kusema, akikaidi maagizo kutoka kwa wafanyakazi wa ndege.

Share: