Idf yasema imefanya mashambulizi 250 ya anga gaza

Jeshi la Israel linasema kuwa limefanya mashambulizi zaidi ya 250 huko Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita.

Maafisa wa Hamas wanasema takriban watu 50 wameuawa katika wimbi la hivi punde la mashambulizi ya anga.

IDF inasema ilizuia jaribio la "kikosi cha kigaidi" katika eneo la Sajaiya karibu na Mji wa Gaza - ngome muhimu ya Hamas - ambayo ilikuwa ikijiandaa kurusha makombora kuelekea eneo la Israeli, lakini shambulio la anga la IDF "liliondoa kikosi hicho".

IDF inasema vikosi vyake vya ardhini, anga, na majini vinaendelea kufanya "mashambulizi mahususi katika maeneo lengwa ya ugaidi na miundombinu katika Ukanda wa Gaza, huku maeneo zaidi ya 250 ya ugaidi yakishambuliwa siku ya mwisho".

Share: