Idadi ya waliopoteza Maisha Kariakoo ni watu wa nne na sio wa Tano - RC Chalamila

Mkuu wa mkoa wa Dar es salam Albert Chalamila, amekanusha taarifa za awali ambazo zilitolewa na kamanda wa Zimamoto Kinondoni mapema hii leo kuwa vifo vilifikia idadi ya watu watano, KWa mujibu wa taarifa rasmi kutoka kwa madaktari vimethibitisha kuwa kufikia sasa ni Vifo Vinne pekee.

Akizungumza na waandishi wa habari na wananchi mbalimbali katika eneo la Kariakoo usiku huu Chalamila amesema “Taarifa iliyothibitishwa na madaktari hadi Sasa waliofariki katika ajali hii ni watu wanne na tunashukuru Mungu idadi ya waliokolewa ni wengi kuliko waliofariki, Pamoja na hayo muda huu bado kazi inaendelea kuingiza oksijeni kwenye floor za chini ambako huko inasadikika bado kuna watu wachache wali kuwepo wakati Jengo linaanguka” amesema Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila.

Ameongeza kuwa “Hadi kufikia sasa tumeokoa watu 70 na wameendelea kupata matibabu Muhimbili, Amana na Mnazimmoja.Katika Idadi hiyo watu 40 walikuwa Muhimbili na 35 kati Yao wamesharuhusiwa tayari”

Share: