Rais Samia tayari amekwishatoa maelekezo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kupitia Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa na Serikali ya mkoa kwamba serikali igharamie mazishi ya waliopoteza maisha.
Baadhi ya miili ya marehemu waliofariki katika maporomoko ya matope katika Wilaya ya Hanang’ mkoa wa Manyara ikiwa katika viwanja vya Shule ya Msingi Katesh kwa ajili ya kuagwa. Mhe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anaongoza zoezi la kuaga miili hiyo leo Disemba 4, 2023.
Mpaka sasa jumla ya watu 57 wamefariki dunia na wengine 85 wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, Hospitali ya Wilaya ya Hanang na Kituo cha Afya Gendabi, kufuatia maafa yaliyoukumbuka mkoa huo.
Aidha Rais Samia tayari amekwishatoa maelekezo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kupitia Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa na Serikali ya mkoa kwamba serikali igharamie mazishi ya waliopoteza maisha, waliopoteza makazi serikali iwape pamoja na kufanya tathmini ya maafa.