Hukumu ya wazazi wa mtoto aliyewapiga wenzake risasi shuleni yaongezwa kufikia kifungo cha miaka 10 jela

Hukumu ya miaka saba ilipendekezwa, lakini waendesha mashtaka waliomba iongezwe.

James na Jennifer Crumbley, wazazi wa kijana huyo walionekana pamoja kwa mara ya kwanza baada ya miezi kadhaa wakati wa kusikilizwa kwa hukumu ya kesi hiyo, Jumanne.

Wote wawili walionyesha majuto juu ya shambulizi lililotekelezwa na mtoto wao, huku mawakili wao wakishinikiza kupunguza kifungo chao gerezani.

Katika kesi hiyo ya kihistoria, majaji tofauti walimpata kila mzazi wa kijana huyo, Ethan Crumbley na hatia ya kuua bila kukusudia mapema mwaka huu.

Jaji Cheryl Matthews alisema kuwa hukumu iliyoongezwa ya miaka 10 hadi 15 ilikuwa "kama onyo" na ilionyesha kushindwa kwa wazazi kusitisha shambulio hilo.

Wazazi hao wanaweza kupata msamaha baada ya kutumikia kifungo cha miaka 10 gerezani, lakini hawawezi kuzuiliwa kwa zaidi ya miaka 15 ikiwa msamaha utakataliwa.

Waendesha mashtaka walidai wawili hao walikuwa wamepuuza dalili za wazi kwamba afya ya akili ya mtoto wao ilikuwa imezorota, na wakabainisha kwamba walimnunulia Ethan Crumbley bunduki aliyotumia katika shambulio la 2021.

Mtoto wao wa kiume alikuwa na umri wa miaka 15 alipowaua wanafunzi wanne kwa bunduki katika Shule ya Upili ya Oxford. Wengine saba walijeruhiwa kwa risasi.

Share: