Hamas yatoa video ya mateka watatu wakiomba usaidizi

Wazee hao wametambuliwa kuwa wakazi wa kijiji cha Nir Oz kilichoko karibu na mpaka wa Israel na Gaza, na ambao walichukuliwa mateka na kundi la Hamas mnamo Oktoba 7.

Wake wa watatu hao ambao pia walikuwa wamechukuliwa mateka wameachiliwa.

Akizungumza kwenye vidio hiyo, mmoja wa wazee hao ameeleza kuwa wote wanaugua magonjwa sugu na wametoa wito wa usaidizi.

Msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari amesema video hiyo inaonyesha "ukatili wa Hamas dhidi ya wazee wasiokuwa na hatia na ambao wanahitaji matibabu."

Mnamo mwishoni mwa mwezi uliopita, Israel na Hamas walibadilishana wafungwa na mateka, huku raia 100 wa Israel waliokuwa wameshikiliwa mateka wakiachiliwa huru wakati wafungwa 240 wa Palestina waliokuwa wamezuiliwa na Israel wakiachiliwa.

Wengi walioachiliwa huru na pande zote wakati huo walikuwa wanawake na watoto.

Share: