Familia itapokea Billion 266 kama fidia mauaji ya ndugu yao

Familia ya mwanaume mweusi (Botham Jean) aliyepigwa risasi na kuuawa nyumbani kwake na Afisa wa Polisi wa Dallas ambaye alisema alidhani mtu huyo amevamia nyumba yake Septemba 26,2018 itapewa karibu dola milioni 100 (sawa na Bilioni 266 za Kitanzania) siku ya Jumatano katika kesi ya madai ya Serikali Kuu, huku kesi hiyo ikiunguruma kwa siku 3 mfululizo.

Mahakama iligundua kuwa Afisa huyo wa zamani Amber Guyger alitumia nguvu kupita kiasi katika kifo cha Botham Jean mwaka 2018 na kukiuka haki zake za kikatiba. Majaji walirejesha hukumu dhidi yake ambapo alipaswa kulipa dola milioni 98.65. Tukio hilo la mauaji liliteka hisia watu wengi kwa sababu ya mazingira yalivyokuwa ikiwa ni miongoni mwa matukio kadhaa za wanaume weusi ambao wamekuwa wakiuawa na Maafisa wa Polisi weupe.

Wakati kesi ikiendelea kusikilizwa, Mawakili wa familia ya Jean (mtu mweusi aliyeuawa) waliiuliza Mahakama kwa kutumia ujumbe wa kwamba wakaazi wa eneo la Dallas watakuwa salama katika nyumba zao, Gazeti la The Dallas Morning News iliripoti. Guyger hakuweza kushiriki kwenye kesi hiyo kutokana na faili za Mahakama, ambazo familia ilisema zilionyesha ukosefu wa uwajibikaji kwa matendo yake.

Tufuatilie kupitia #STBongoTV ndani ya kisimbuzi cha @startimestz CH 161 (antena) CH 401 (Dish) pamoja na kwenye YouTube channel yetu ya #STBongoTV Kwa Taarifa zaidi.

#STBongoUPDATES #NyumbaniKwanza

Share: