Ecuador: watu waliojifunika nyuso wavamia studio za tc television

Wanaume waliojifunika sura zao wamevamua Studio ya TV (TC Television) ya Umma katika Mji wa Guayaquil wakiwa na silaha za moto na marungu wakati wa matangazo yakiwa mubashara kisha kuwateka Wafanyakazi wa kituo hicho kwa muda.

Imeelezwa hakuna mtu aliyeuawa katika tukio hilo ambalo lilizimwa na Vyombo vya Usalama vilivyofika kituoni hapo na kufanikiwa kuwaweka chini ya ulinzi Watuhumwa 13 ambao watafunguliwa mashtaka ya Ugaidi licha ya Mamlaka kutoweka wazi nani yupo nyuma ya pazia na lengo la watekaji.

Watazamaji walishuhudia kilichokuwa kikiendelea mubashara kwa dakika 15 baada ya watu hao kuingia studio kisha matangazo yakakatika.

Share: