Dkt. tulia ackson amekabidhi nyumba mbili wilaya ya rungwe

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 30 Disemba, 2023 amekabidhi nyumba mbili kwa Wakazi wa Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya ambazo zimejengwa kupitia taasisi yake ya Tulia Trust.

Wanufaika katika nyumba hizo ni Bi. Neva Kisulu mkazi wa Kijiji cha Kibisi Kata ya Kyimo ambaye amekuwa akiishi katika mazingira magumu kutokana na maradhi yanayomkabili pamoja na Ndg. Ambele Wilfred mkazi wa Kijiji cha Kibisi ambaye ni mlemavu wa viungo.

Share: