Dkt. mpango azindua rasmi mradi wa umeme wa ijangala wa 360 kw

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amezindua rasmi Mradi wa Kufua Umeme wa Maji Ijangala wa Kilowati 360, unaomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kusini Kati katika kijiji cha Masisiwe Wilaya ya Makete Mkoani Njombe.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo, Dkt. Mpango ameelezea kufurahishwa kwake na uwepo wa Mradi, na kuwataka Wadau wengine kujitokeza kuwekeza kwenye miradi ya namna hiyo katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na umeme wa kutosha, wa uhakika na wa bei nafuu.

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ameiagiza Wizara ya Nishati kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa Mradi wa Rumakali ili kuongeza upatikanaji wa Umeme Wilayani Makete.

Akizungumza wakati wa Hafla hiyo. Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga, amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa, Wizara ya Nishati inaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha vijiji vyote vinafikiwa na Umeme kwa wakati na kuwa kwa Wilaya ya Makete wanakaribia kumaliza kupeleka umeme kwa vijiji vyote 98

Share: