Dcea: tuna orodha ya wasanii wanaotumia dawa za kulevya, tutawapima

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewataka Wasanii wanaotumia Dawa za Kulevya kuacha mara moja huku akieleza ujenzi wa Maabara mpya ya Ukaguzi na Sayansi Jinai unakamilishwa na Wasanii hao watapimwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria

Lymo amesema “Nitoe wito kwa Wasanii wanaotumia Dawa za Kulevya tuna orodha yao, tuna orodha ya wanaovuta Bangi, wanaovuta Heroin na Cocaine, tunawapa muda wa kujirekebisha, mitambo yetu ya Maabara ikikamilika tutawapima na tukijiridhisha mnatumia mtachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa Mahakamani”

Share: