Daraja muhimu maryland, limeanguka mtoni baada ya kugongwa na meli ya kontena

Daraja muhimu huko Baltimore, Maryland, limeanguka mtoni baada ya kugongwa na meli ya kontena, huduma za uokoaji zimesema.

Msemaji wa Idara ya Zimamoto ya Jiji la Baltimore anasema daraja hilo liliporomoka kwenye Mto Patapsco baada ya kugongwa na chombo hicho mapema asubuhi ya leo.

Operesheni ya uokoaji ya mashirika mengi kwenye eneo la tukio inaendelea.

Chifu Kevin Cartwright, mkurugenzi wa mawasiliano wa Idara ya Zimamoto ya Jiji la Baltimore alituthibitishia kuwa daraja hilo lilikuwa limegongwa na "meli kubwa".

Pia alituambia kwamba "watu kama saba na magari kadhaa" yameanguka mtoni.

Share: