Daktari wa kenya anayehusishwa na kundi la kigaidi la islamic state amehukumiwa miaka 12 jela

Daktari wa Kenya anayehusishwa na kundi la kigaidi la Islamic State amehukumiwa miaka 12 jela kwa kupanga shambulio kubwa la kibaiolojia yapata miaka minane iliopita.

Mohammed Abdi Ali alikuwa anapanga kutumia virusi vya kimeta kutekeleza shambulio hilo lakini alikamatwa kufuatia taarifa ya wananchi kwa polisi.

Ali pia alikuwa na hatia ya kuwahusisha vijana hao na wapiganaji wengine wa Islamic State nchini Libya.

Alikamatwa pamoja na watu wengine wawili ambao waliachiliwa kwa kukosa ushahidi.

Hakimu alisema kwamba aliangazia kuhusu miaka 8 aliyokuwa gerezani.

Share: