Dada wa muigizaji wema sepetu, sunna sepetu akutwa na kesi ya utakatishaji fedha nchini marekani

Waafrika wawili, wakazi wa Massachusetts, nchini Marekani wamepatikana na hatia ya utakatishaji fedha na kujipatia fedha hizo kwa njia ya udanyanyifu.

Sunna Sepetu mwenye umri wa miaka 37, ambaye pia dada wa Wema Sepetu, aliyekuwa Miss Tanzania kwa mwaka 2006, na mwenzake Nafise Quaye kutoka Nigeria wamekutwa na hatia hizo mbele ya Mwanasheria wa Marekani Jane E. Young, huku hukumu yao ikipangwa kutolewa Julai 8, 2024.

Wawili hao wanakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 jela.

Ilidaiwa kuwa, kati ya mwaka 2013 na 2019, washitakiwa hao walipokea kiasi cha dola milioni 3.2 kutoka kwa mwathiriwa wa utapeli kutoka Jimbo la Texas. Fedha hizi zilitumwa kwenye akaunti za benki zilizoanzishwa na washitakiwa kwa ajili ya kampuni mbalimbali hewa. Kisha washitakiwa walihamisha fedha hizo za udanganyifu kwa kiongozi wa kikundi cha utapeli wa fedha, ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.

Pia, ilibainika kuwa wawili hao wamekuwa wakijuhusisha na mitandao ya kitapeli kwa muda mrefu sasa.

Share: