Christina chapman ameshtakiwa kwa kuwasaidia wakorea kaskazini kupata kazi nchini marekani

Mkazi huyo wa Arizona anadaiwa kuiba vitambulisho vya raia wa Marekani

Waendesha mashtaka wa Marekani wamemshutumu mwanamke wa Marekani kwa kuwasaidia Wakorea Kaskazini kupata kazi nchini Marekani wakiwa mbali na kisha kuwatumia mishahara yao Korea Kaskazini.

Christina Chapman anashtakiwa pamoja na raia watatu wa Korea Kaskazini kwa kushiriki katika njama hiyo ya kina.

Mkazi huyo wa Arizona anadaiwa kuiba vitambulisho vya raia wa Marekani, kisha kuwasaidia wafanyakazi wa kigeni wa Teknolojia ya Mawasiliano kutumia vitambulisho hivyo kujifanya Wamarekani na kupata ajira katika makampuni ya Marekani, kulingana na waendesha mashtaka.

Bi Chapman ameshtakiwa kwa makosa tisa ya kula njama ya kuilaghai Marekani.

Wachunguzi walisema mpango huo "wa kushangaza" ulitumia vitambulisho vilivyoibiwa vya watu 60, na kuzalisha karibu $7m katika fedha ambazo zilirejeshwa Korea Kaskazini, ikiwezekana kuchangia mpango wa silaha nchini humo.

Mpango huo - unaohusisha baadhi ya makampuni 300 ya Marekani - unadaiwa kuanza Oktoba 2020. Kulingana na hati ya mashtaka, wafanyakazi walikuwa "wafanyakazi wenye ujuzi wa hali ya juu ya teknolojia ya habari (IT)."

Kampuni hizo, ambazo hazikuwa na ufahamu wa mpango huo, hazikutambuliwa, lakini maafisa walisema ni pamoja na kampuni kadhaa za Fortune 500, pamoja na mtandao mkubwa wa TV, kampuni ya ulinzi ya indicta, kampuni ya teknolojia ya "Silicon Valley" na "mtaalamu" wa utengenezaji wa magari.

Share: