China: ukosefu wa ndoa wafanya kina mama kuwawatafutia mabinti zao waume

Chen amekuwa akiunganishwa kwa dhifa za chakula kufahamiana na wachumba mara zaidi ya 20, zote zikiwa zimepangwa na mama yake.

Baadhi ya tarehe zimekuwa mbaya zaidi kuliko zingine, anasema, kwa sababu ana hali ambayo wanaume wengi ambao ameonana nao wanaonekana hawawezi kuikubali: hataki watoto.

"Kupata watoto kunachosha sana na sipendi watoto," anasema Chen, ambaye yuko katika miaka yake ya 20 na anataka tu kutaja jina lake la mwisho. "Lakini haiwezekani kupata mwanamume ambaye hataki kupata watoto. Kwa mwanaume kutozaa... Ni sawa na kumuua."

Licha ya kuwa na dhifa kufuatana za kukutana na wachumba ambazo hazijafanikiwa, shinikizo la kuoa bado halijapungua. Inamfanya kuwa tayari "kulipuka," anasema.

Sio tu wazazi wa Chen wanaotaka aolewe na kupata watoto. Viwango vya ndoa na kuzaliana vinapoporomoka, Chama cha Kikomunisti cha China kinawahimiza mamilioni ya vijana wa kike na wa kiume kubadili mwelekeo huo.

Mwaka jana, idadi ya watu wa China ilipungua kwa mara ya kwanza katika miaka 60, na kiwango cha uzazi kilishuka hadi rekodi ya chini. Idadi ya ndoa zilizosajiliwa pia haijapungua kufikia hivi (milioni 6.83) tangu 1986.

Wakiwa wamekatishwa tamaa na kuzorota kwa uchumi na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira, vijana wa China pia wanaondokana na chaguzi za wazazi waoza tangu jadi.

Wasiwasi huo umemfikia Xi, ambaye hivi karibuni alitoa hotuba kuhusu umuhimu wa utamaduni wa ndoa na uzazi. Pia alizungumzia "kuimarisha miongozo" ili kuunda maoni mapya ya vijana kuhusu ndoa, watoto na familia.

Sio kwamba maafisa wa China hawajajaribu, Kote nchini, warasimu wameacha kuhimiza vijana kuoa na wanandoa kubaki kwenye ndoa na kupata watoto.

Mapema mwaka huu, mji mdogo katika mkoa wa mashariki wa Zhejiang ulitangaza kuwa utawapa wanandoa Yuan 1,000 ($137) kama "zawadi" ikiwa bibi arusi alikuwa na umri wa miaka 25 au chini.

Tangazo hilo liliwashangaza na kuwakasirisha wakaazi, ambao waliita serikali ya eneo hilo kuwa ‘wajinga’ kwa kudhani kwamba pesa kidogo kama hiyo inaweza kuathiri uamuzi muhimu kama huo.

Zaidi ya hayo, maafisa walisisitiza juu ya "kipindi cha tafakari cha siku 30" kwa wanandoa ambao walitaka kutengana au talaka. Hii ilizua wasiwasi kwamba chaguzi za kibinafsi zinaweza kuwekewa vikwazo na wanawake wanaopitia unyanyasaji wa nyumbani wanaweza kudhurika.

Katika maeneo ya mashambani, ambako wanaume wengi zaidi wanatatizika kupata wachumba, mamlaka imewaamuru wanawake kuacha kuomba mahari - kiasi ambacho bwana harusi wa siku zijazo au wazazi wake hulipa kwa familia ya mke wake wa baadaye kuonyesha kujitolea.

Kama "vishawishi" vingine, hii pia haitafanya kazi, anasema mwanauchumi Li Jingkui.

Hata bila mahari, wanaume bado wanapata ushindani mkubwa. "Kunaweza kuwa na njia zingine za kushindana: kama nyumba, magari au mwonekano bora."

Wataalamu wanasema viongozi wa China, wengi wao wakiwa wanaume, hawawezi kuelewa ni nini kinachochochea vijana kuanza kuchangua sana, hasa wanawake.

Juhudi za wanaume hawa, na wale wote walio chini yao, mara nyingi huchukuliwa kuwa potofu na hata za juu juu, na kwa hivyo hudhihakiwa mtandaoni.

"Maafisa wote wa serikali wana wake," Li anasema. "Hawaelewi maumivu haya."

Wataalamu wanaamini kwamba idadi ya watu pekee ya China inaundwa na makundi mawili yasiyolingana: wanawake wa mijini na wanaume wa vijijini.

Wanaume wa mashambani hukabiliana na matarajio ya kiuchumi, kama vile bei ya juu ya mahari na kazi nzuri ambayo itampa hakikisho maishani la kumwezesha kukidhi mahitaji ya familia.

Na hii, kwa upande wake, inaonekana kuwasukuma wanawake katika maeneo ya vijijini kuchukua muda zaidi wakati wa kuchagua mpenzi.

"Niliporudi nyumbani kwa Mwaka Mpya wa Kichina, nilihisi vizuri kuwa mwanamke katika soko la wanaowezakuolewa vijijini Uchina ," anasema Cathy Tian, 28, anayefanya kazi Shanghai.

Anasema alikuwa na wasiwasi kuhusu kuchukuliwa kuwa "mzee kidogo" katika jimbo la kaskazini la Anhui, ambapo kwa kawaida wanawake huolewa wakiwa na miaka 22 akabaini kumbe ni mambo ni kinyume na fikra hizo.

"Sihitaji kuchangia chochote zaidi ya mwanamume kuwa na nyumba, gari, sherehe ya kuonyesha kujitolea na kulipa mahari. Nilihisi kuwa thamani sana katika soko hili la ndoa."

Wanawake wa mijini, kwa upande mwingine, wanasema kinachowatia wasiwasi ni kuongezeka kwa pengo kati ya jinsi wanavyoiona ndoa na jinsi jamii inavyoitazama.

"Sina wasiwasi," Chen anasema. "Wasiwasi wangu unatoka nje."

Tofauti na kizazi cha wazazi wake, wakati maisha yalikuwa changamoto huku kupenda ikiwa anasa, watu na wanawake sasa wana chaguzi nyingi zaidi, anasema.

"Wazo letu sasa ni kwamba ni sawa kutokuwa na watoto na kwamba sio wajibu tena."

Wanawake pia wanaeleza kuwa, kama ulimwengu unaowazunguka, kampeni za serikali zinalenga wanawake na kupuuza wajibu wa wanaume kama washirika, Na matarajio yasiyo sawa yanawaondoa kutoka kwa wazo la kuwa wazazi.

Share: