Bus la Ally's lagonga Kichwa cha Treni Manyoni Singida

Ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Ally's Star lenye namba T.178 DVB likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kugonga kichwa cha Treni katika makutano ya reli na barabara, nje kidogo ya Mji wa Manyoni Mkoani Singida, imesababisha vifo vya Watu 13 na kujeruhi wengine 25.

Police wanaendelea kuchukua manusura na maiti kupeleka Hospital ya karibu hapa Singida.

Chanzo inasemekana ni kichwa cha train kupita kikiwa hakijawasha taa wala kupiga horn. Na inasemwa hii si mara ya kwanza. Na mpaka hapo kichwa kinaonekana taa ikiwa haijawaka. Kinanguruma tu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Singida, ACP Stella Mutabihirwa amesema “Ajali imetokea leo Novemba 29, 2023 Saa 10 Alfajiri, basi lilikuwa na Watu 57, idadi ya majeruhi na vifo ni mpaka muda huu (asubuhi), kichwa cha Treni kilichohusika kina namba za usajili V1951-9006 kilikuwa kikitokea Itigi kuelekea Manyoni.”

Share: