Burkina faso: watu zaidi ya 10 wamefariki kwa kupigwa risasi

Inadaiwa waliofanya shambulizi ni sehemu ya Makundi ya Waasi ambao pia wamekuwa wakiwalenga Wanajeshi

Zaidi ya Watu 10 wameuawa kwa kupigwa risasi wakiwa msikitini katika Mji wa Natiaboani siku ambayo pia iliripotiwa Watu 15 (Februari 25, 2024) wameuawa kwa kushambuliwa wakiwa Kanisani (Mji wa Essakane) ikiwa ni mwendelezo wa machafuko yanayotokea

Inadaiwa waliofanya shambulizi ni sehemu ya Makundi ya Waasi ambao pia wamekuwa wakiwalenga Wanajeshi na Wanamgambo wa kujilinda ambao alikuwa eneo la tukio

Aidha, inaelezwa Ripoti ambazo hazijathibitishwa zilizopo kwenye Mitandao ya Kijamii zinaonesha idadi ya waliokufa kutokana na shambulio la Msikiti inaweza kuwa kubwa zaidi kuliko hesabu iliyotolewa na Mamlaka

Burkina Faso ipo chini ya Utawala wa Kijeshi ambao ulichukua Mamlaka miaka miwili iliyopita na kuahidi kushinda vita dhidi ya Waasi lakini ghasia zinaendelea

Share: