Burkina faso: takriban watu 170 wameripotiwa kuuawa na waasi

Takriban Watu 170 kutoka Vijiji vya Komsilga, Nodin, na Soro katika Mji wa Yatenga, wameripotiwa kuuawa na Waasi wanaohusishwa na Vikundi vya al Qaeda na IS

Taarifa iliyotolewa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Machi 3, 2024 imeeleza kuwa mauaji hayo yaliyoanza Wiki iliyopita yalihusisha Watu 17 waliokutwa Kanisani na maeneo mengine ya mikusanyiko katika Vijiji hivyo

Amesema tayari uchunguzi wa kina umeanza juu ya tukio hilo ambalo ni mwendelezo wa matukio ya Ukatili na Unyanyasaji unaotajwa kuhusisha masuala ya Kidini ambayo yamekuwa yakisababisha machafuko na vifo kwa zaidi ya miaka 10 ikiwemo Watu zaidi ya Milioni 2 kuyakimbia makazi

Share: