Brazil: mwanamke ampeleka maiti benki ili apate saini ya mkopo wa fedha

Mwanamke mmoja nchini Brazil amezua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii baada ya kupeleka maiti ya mzee katika benki, akitarajia kupata saini ya mkopo.

Katika video iliyosambazwa mitandaoni mwanamke huyo alionekana akisukuma maiti ya mzee iliyekuwa imevishwa nguo nadhifu na kukalishwa kwenye kiti cha magurudumu hadi kwenye eneo la wateja kuhudumiwa na kujaribu kumfanya atie saini karatasi iliyokuwa mbele yake.

Alimpa kalamu na kujaribu kumuita asaini karatasi hiyo lakini hakuweza kufanya hivyo.

Wafanyakazi wa benki waliotilia shaka ustawi wa mwanamume huyo huko Rio de Janeiro walipiga simu polisi katika hatua iliyomfanya mwanamke huyo kukamatwa kwa madai ya ulaghai.

Share: