Bohari ya dawa (msd) imeongeza majokofu na vifaa tiba hanang

Hatua hii ni muendelezo wa MSD kuwasilisha bidhaa za afya kwa ajili ya kusaidia maafa yaliyojitokeza katika wilaya ya Hanang.

Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) imeendelea kuongeza vifaa na bidhaa zinazohitajika kusaidia maafa yaliyotokea mkoani Manyara.

Leo hospitali ya Wilaya ya Hanang (Tumaini) imepokea majokofu mawili ya kuhifadhia miili ambapo kila moja ina uwezo wa kuhifadhi miili sita(6) kuongeza kwenye majokofu waliyokuwa nayo awali.

Hatua hii ni muendelezo wa MSD kuwasilisha bidhaa za afya kwa ajili ya kusaidia maafa yaliyojitokeza katika wilaya ya Hanang.

Timu ya MSD ipo wilayani humo kupokea mahitaji na kuhakikisha mahitaji hayo yanafika eneo la tukio.

Share: