Halmashauri ya Jiji la Dar es Salam imetenga jumla ya Shilingi bilioni 4.1 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Kitunda Relini ambapo shilingi million 528 ni fedha kutoka Mpango wa kuboresha elimu ya Sekondari(Secondary Education Quality Improvement Program.SEQUIP) huku zaidi ya Bilioni 3 ikiwa ni fedha kutoka Serikali kuu na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 29, 2024 na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Ndg. Elihuruma Mabelya wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa Shule hiyo iliyofanyika katika Kata ya Kitunda Jijini Dar esSalaam .
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe.Omary Kumbilamoto amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuwa mwadilifu kwa kuhakikisha anakamilisha mradi kwa wakati huku akimisisitiza ashirikiane na wataalamu kutoka Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam katika kazi ili kuleta matokeo yenye tija kwa maslahi ya Wananchi.
Aidha Mhe. Kumbilamoto amemshukuru Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha anazoendelea kutoa kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo huku akiwahakikishia wananchi kuwa mradi utakamilika kwa muda uliopangwa na kwa ubora uliokusudiwa.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia na Habari ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe. Jerry William Silaa ametoa wito kwa Mstahiki Meya na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuweka mifumo bora ya kumsimamia mkandarasi ili kazi ya ujenzi ikamilike kwa wakati na ubora ili wanafunzi waanze kutumia Shule hiyo na kupunguza msongamano darasani huku akimtaka mkandarasi aliyepewa tenda kufanya kazi hiyo kwa bidii na kwa viwango ili kuleta matokeo yenye tija kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndg. Elihuruma Mabelya Amesema “Serikali ya Awamu sita chini ya Rais Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan inatuletea pesa nyingi katika Halmashauri yetu ni wajibu wetu kuhakisha Fedha zinatumika kwa kazi iliyokusudiwa kwa maendeleo ya jamii yetu.