Serikali imefanikiwa Kununua vitendea kazi kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini vyenye Thamani ya Bilioni 280, kupitia mkopo nafuu, ambao umeidhinishwa ili kufanikisha adhma ya Jeshi hilo ya Kulinda maisha na mali za watanzania ambapo vitendea kazi hivyo vitaanza kuwasili nchini Aprili 2025
Hayo yamebainishwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini CGF John Masunga kwenye Hafla ya awali kwa askari wapya 221, Kozi namba 5, 2024 ambapo kuwasili kwa vifaa hivyo itakuwa ni historia kwa Jeshi hilo kununua vitendea kazi vingi kwa mara moja.
CGF Masunga amesema baadhi ya Vitendea kazi vitakavyonunuliwa ni pamoja na Magari 150 ya Zimamoto na Uokoaji, ambapo Utekelezaji wa mkataba huo umeanza kutekelezwa.
Share: