Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa Kagera kumsimamia Mkandarasi M/s Abemulo Contractors Ltd afanye kazi usiku na mchana ya ujenzi wa upanuzi wa njia nne wa barabara ya Bukoba (Rwamishenye) - Bukoba Port (km 5.1), sehemu ya kwanza yenye urefu wa kilometa 1.

Bashungwa ametoa agizo hilo leo tarehe 28 Oktoba 2023 Bukoba mkoani Kagera wakati akikagua kuanza kwa kazi ya Ujenzi wa upanuzi wa Barabara hiyo ya njia nne sehemu ya kwanza inayoanzia Roundabout ya Rwamishenye hadi eneo la Mitaga lenye urefu wa Kilometa 1.
Bashungwa amesema kuanza kazi ya upanuzi wa barabara hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango aliyoyatoa kwa TANROADS ya kukabiliana na ajali za mara kwa mara zinazotokea kwenye mteremko wa Nyangoye katika barabara hiyo