Baadhi ya wananchi wanadai utawala wa rais ruto umekuwa kinyume na ahadi zake

Malalamiko mengine ni pamoja na Kodi na Tozo zinazokusanywa zimekuwa zikisaidia kufadhili ubadhirifu Serikalini badala ya kuboresha huduma

Hatua hiyo inafuatia ongezeko la Kodi na Tozo mbalimbali zilizopitishwa kupitia Sheria mpya ya Fedha ya mwaka 2023, Sheria ambayo imelalamikiwa kuongeza mzigo wa gharama za maisha kwa Wananchi.

Kupitia mitandao ya Kijamii baadhi ya Wananchi wanadai Utawala wa Rais Ruto umekuwa kinyume na ahadi zake za kushusha gharama za maisha badala yake Rais ameongeza mzigo wa Kodi kwenye bidhaa na vipato vya Wananchi kiasi ambacho wanamlinganisha na Zakayo Mtoza Ushuru aliyetajwa katika Biblia.

Malalamiko mengine ni pamoja na Kodi na Tozo zinazokusanywa zimekuwa zikisaidia kufadhili ubadhirifu Serikalini badala ya kuboresha huduma za umma. Pia, Wananchi wamedai Safari za Rais zimekuwa nyingi na zinatumia Kodi zao kwa manufaa yasiyoonekana.

Tangu Julai 2023, kumekuwa na ongezeko la Kodi kwa Mishahara ya kila mwezi kutoka 30% hadi 35%, Kodi ya Nyumba 1.5%, Mfuko wa Bima 2.75%, Ushuru wa Mauzo ya 3%, Kodi ya Mafuta 16% kutoka 8%. Ongezeko hilo liliibua Maandamano yaliyosabbaisha baadhi ya Watu kuuawa.

Share: