Askari wapya 221 wahitimu mafunzo ya awali zimamoto na uokoaji

Askari wapya 221 wahitimu mafunzo ya awali zimamoto na uokoaji, Dkt Maduhu Kazi ataka utii wa Kiapo na nidhamu kwa askari wapya zimamoto na uokoaji

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Dkt Maduhu Kazi amewataka Askari wapya wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuheshimu kiapo walichoapa pamoja na kuzingatia nidhamu ndani ya Jeshi hilo kwani Serikali haitovumilia vitendo vya utovu wa nidhamu ambapo watakuwa wamekiuka kiapo hicho



Dkt Kazi ametoa wito huo wakati akifunga mafunzo ya awali kwa askari wapya 221 kozi namba 5, 2024 iliyofanyika kwenye chuo cha Mafunzo ya Zimamoto na Uokoaji Chogo iliyopo Handeni, Mkoani Tanga 

Aidha Amemtaka Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini CGF John Masunga kuendelea kusimamia nidhamu kwa askari wote, ambapo pia amewapongeza wahitimu kwa mchango mkubwa kwa kuonesha uzalendo chuoni hapo


Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Zimamoto na Uokoaji Chogo, Mrakibu Kamila Labani amesema Jumla ya Askari 221 wameweza kuhitimu mafunzo ya awali huku wanafunzi watano wakishindwa kuhitimu kutokana na Changamoto ya Nidhamu, utoro na Afya


Share: