Askari ashtakiwa kwa kumpiga na kumkamata mtu mweusi

Mwanaume mmoja na baba wa watoto wanne (Silvester Hayes) amemshtaki Askari wa Dallas PD na Maafisa kadhaa baada ya kukamatwa kimakosa na kupigwa kikatili wakati aliposimama kwa bahati mbaya kwenye taa za trafiki. Silvester Hayes alikuwa akiendesha gari wakati alipoenda kununua vifungua kinywa kwa ajili ya watoto wake wakati Maafisa wa Askari wa Dallas Walter Paul Guab na Holly Harris walipomsimamisha kwa kushindwa kufuata sheria za taa za barabarani (ishara ya kusimama).

Hayes alitoa ushirikiano kwa kutoa leseni yake ya udereva kwa Afisa Guab na kumjulisha kuwa alikuwa na bunduki iliyosajiliwa kihalali ndani ya gari. Badala ya kutumia leseni yake kupata taarifa zake kupitia kompyuta, Afisa Harris alimweleza Afisa mwenzake (Guab) kuwa walikuwa wakimtafuta mshukiwa anayeitwa "Sylvester," ambaye alikuwa na makosa ya unyanyasaji wakati huo. Maafisa wote wawili walijikuta wakimdhania Silvester kuwa ndiye “Sylvester.”

Bila kujiridhisha na usahihi wa juu ya mshukiwa waliyekuwa wanamtafuta, Askari hao wakiwa wanaendelea na mapishano na mwanaume huyo, maofisa wengine walifika kwenye eneo la tukio, na kuanza kumpiga, na kumlazisha Hayes kuingia ndani ya gari la Polisi na baadae kumpeleka nyuma ya gari hilo wakati ambapo Afisa Harris aliangalia leseni yake na kuthibitisha kuwa mwanaume huyo siye mtuhumiwa waliyekuwa wanamtafuta, " Duuh tumemkamata mtu ambaye sio mhalifu!"

Badala ya kumwachilia kufuatia mkanganyiko huo, kwa mujibu wa Hayes (mtu mweusi anayeonekana kwenye video), bado waliashikiria kwa kupinga kukamatwa na walipekea Kituo cha Polisi ambapo alikaa ndani kwa siku kadhaa. Kutokana na kitendo cha kukamatwa huku ingawa ilikuwa ni kimakosia, Hayes anasema alipoteza kazi yake, nyumba yake, na uwezo wake wa kuhudumia watoto wake.

Share: