Arusha na Sweden zakubaliana kuendelea kushirikiana kukuza sekta ya elimu mkoani Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda Leo Jumatano Novemba 20,2024 Jijini Arusha amekutana na kuzungumza na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Charlotta Ozaki Macias na kukubaliana kuendeleza mahusiano ya muda mrefu yaliyopo kati ya pande hizo mbili hasa katika kuwanufaisha Raia wa pande hizo


Balozi Charlotta akiambatana na wadau wa Shirika la Kimataifa kutoka Umoja wa Ulaya linalotoa ufadhili wa elimu (GPE) wapo Mkoani Arusha kukagua miradi mbalimbali ya elimu inayosimamiwa na GPE, ikitoa zaidi ya Bilioni 4 kwaajili ya kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu mkoani Arusha, ambapo Mhe. Makonda ameahidi kuhakikisha kuwa miradi hiyo inafanya kazi kama ilivyotarajiwa.


GPE inaongozwa na Mwenyekiti wa bodi Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete linatoa ufadhili wa elimu kwa wadau mbalimbali katika kuimarisha mifumo bora ya elimu kwa nchi zaidi ya 89 ikiwemo Tanzania, ambapo huyaweka pamoja mataifa yanayoendelea, wafadhili, mashirika ya kimataifa na sekta binafsi na Umma ili kusaidia uboreshaji wa Elimu kote duniani.

Share: