Aliyemgonga trafiki adakwa na polisi

JESHI la Polisi mkoani Mwanza, linamshikilia Dereva wa gari la Shule ya Msingi Nyamuge, Philipo Mina kwa tuhuma za kumgonga na kumsababishia kifo Askari Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, Sajenti Stella Alphonce eneo la Nyamuhongolo wilayani Ilemela.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, SACP. Wilbroad Mutafungwa amesema Askari huyo alisimamisha gari kwa ukaguzi, baadaye gari lilikutwa na kosa na kumtaka Dereva arudishe gari nyuma kwa ajili ya usalama, ndipo alimgonga Askari huyo kwa nyuma na kusababisha kifo chake.

“Dereva wa gari hilo tunamshikilia kwa mahojiano pamoja na gari, mwili wa Askari umehifadhiwa Hospitali ya Bungando” amesema Kamanda huyo.

Share: