Aliye mvamia hakimu alitakiwa apigwe risasi

Hakimu maarufu duniani Jaji Judy amezungumza kuhusu tukio la mshtakiwa Deobra Delone Redden ambaye aliruka juu ya benchi na kumvamia Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Clark County Mary Kay Holthus katika chumba chake cha mahakama wiki iliyopita na kudai alitakiwa apigwe risasi

Katika mahojiano maalum, Jaji Judy alitoa mawazo yake kuhusu video hiyo inayosambaa kwenye mtandao wa kijamii na kusema, “Nilishangaa sana mshtakiwa huyu kufikia hatua aliyofikia bila mtu kumpiga risasi, lakini pengine ilitokea haraka sana hata mara moja kulikuwa na watu wengi sana. Kwa kweli nilishtuka kwamba mtu alifanikiwa kumkaribia hakimu”

Share: