Ziwa tanganyika kufungwa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia tarehe 15 mei

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Ameeleza kwamba Ziwa Tanganyika linamilikiwa na nchi tatu, Zambia, Congo na Tanzania, na hii ya kufunga tarehe 15 Mei ni mkataba wa kimataifa dhidi ya nchi hizi zinazozunguka Ziwa Tanganyika kwamba ifikapo Mei 15 lazima ziwa lote lifungwe katika nchi zote."

"Na ukweli ni kwamba sisi Tanzania pamoja na kwamba mkataba huu tulisaini lakini hatujawahi kuutekeleza lakini wenzetu wamekuwa wakifunga ziwa, na sisi tukasema kwa mwaka huu tuanze kuutekeleza kuanzia Mei 15 kwa muda wa miezi mitatu.” – Alexander Mnyeti, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi

Share: