Ziara ya dharura katika mitambo ya kufua umeme ya kidatu kufuatia kufeli kwa mfumo wa gridi ya taifa

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amefanya ziara ya dharura katika mitambo ya kufua umeme ya Kidatu, Mkoani Morogoro kufuatia kufeli kwa mfumo wa Gridi ya Taifa kwa kusababisha Mikoa mingi Tanzania Bara na Zanzibar kukosa umeme.

Akiwa kwenye kituo cha Kidatu Biteko amewataka TANESCO Kuhakikisha wanatafuta suluhisho la kufeli kwa mfumo wa Gridi ya Taifa mara kwa mara kwa kuhakikisha wanafanya upembuzi wa kina ili kuboresha miundombinu kwenye Gridi hiyo na kuongeza kuwa matatizo kama hayo yanapojitokeza yawe funzo yasijitokeze tena.

“Nawaomba radhi sana Wananchi na Watanzania kwa ujumla kufuatia hitilafu hiyo kwenye mfumo wa Gridi, kwani imeleta usumbufu na changamoto kwa wananchi kutokana na shughuli nyingi za kiuchumi kusimama, kutokana na kutegemea zaidi umeme, na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kwa kuchukua hatua za haraka kufika kwenye eneo la changamoto bila kusukumwa bali kwa kujiongeza.

Aidha, Dkt Biteko, ametoa wito kwa Mkurugenzi wa TANESCO kuhakikisha timu yote ya wataalamu inashirikiana na wananchi ili kupata umeme na kuondoa changamoto hiyo na kuwapongeza kwa kufanya kazi usiku na mchana na hivyo kuhakikisha wananchi wanapata umeme na kumpongeza Mkurugenzi mtendaji wa TANESCO kwa kuchukua hatua za haraka kufika kwenye eneo la changamoto zilizojitikeza kwenye mashine za kufua umeme.

Pia, amewatahadharisha TANESCO kuchukua tahadhari hususan katika kipindi hiki cha kiwango kikubwa cha mvua zinazonyesha na kuwataka TANESCO kuchukua tahadhari kwani maji yanayoingia kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme ni kikubwa na kutolea mfano wa kituo cha kuzalisha umeme cha Julius Nyerere ili kuondoa madhara yanayoweza kusababishwa na wingi wa maji hayo.

Share: