Aidha, Januari 23, 2024 Simai alisema kuna athari zimeanza kujitokeza na kuzua sintofahamu ya kurudisha nyuma Biashara ya Utalii Zanzibar
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohamed Said, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na "Mazingira yasiyo rafiki kwa kazi"
Sehemu ya Barua ya kujiuzulu aliyomtumia Rais Dkt. Hussein Mwinyi imesomeka “Kutokana na imani yangu kwamba jukumu namba moja la Wasaidizi wa Mheshimiwa Rais wakiwemo Mawaziri ni kumsaidia kutekeleza Ilani ya Chama, na inapotokea Mazingira yasiyo rafiki katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ustawi wa Wananchi, ni vyema kutafuta jawabu kwa haraka ili kazi ya kuwaletea Wananchi maendeleo iweze kuendelea, na hata ikibidi kukaa pembeni"
Aidha, Januari 23, 2024 Simai alisema kuna athari zimeanza kujitokeza na kuzua sintofahamu ya kurudisha nyuma Biashara ya Utalii Zanzibar, kufuatia uhaba wa Pombe katika Hoteli na Migahawa ya Watalii, baada ya madai kuwa Bodi ya Vileo imebadilisha Wakala wa Vileo Visiwani humo