Zanzibar: dkt. samia suluhu amekutana na rais yoweri museveni na rais william ruto walipowasili ikulu ndogo tunguu zanzibar march 14, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuongea na Wageni wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais William Ruto wa Kenya walipowasili Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar March 14, 2024.

Kwenye mazungumzo yao wamezungumzia masuala ya mtangamano wa Afrika Mashariki hususan umuhimu wa kuharakisha zoezi la kukusanya maoni ya Wananchi Juu ya muundo na maeneo ya kuangaliwa katika Rasimu ya Katiba ya Fungamano la kisiasa la Afrika Mashariki (EAC Political Confederation).

Zoezi hilo limeshafanyika katika Nchi za Burundi, Uganda na Kenya na linatekelezwa na Timu ya Wataalamu inayoundwa na Wajumbe watatu kutoka kila Nchi Mwanachama.

Share: