Somalia imetaja mpango huo kuwa ni kitendo cha "uchokozi" na kumrudisha nyumbani balozi wake mjini Addis Ababa.
Waziri wa Ulinzi wa jamhuri iliyojitangazia uhuru ya Somaliland amejiuzulu akilalamikia mpango wa kuipa Ethiopia ufikiaji wa bandari katika eneo lililojitenga la Somalia.
Abdiqani Mohamoud Ateye alimkosoa Rais wa Somaliland Muse Bihi Abdi "kwa kutoshauriana na baraza la mawaziri kuhusu makubaliano ya bandari na Ethiopia", akisema "walisikia kuhusu hilo kutoka kwa vyombo vya habari".
Bw Ateye anatokea eneo la Awdal nchini Somaliland, ambako Ethiopia inaripotiwa kutaka kuweka kambi yake ya kijeshi katika mji wa pwani wa Lughaya.
Mkataba wa maelewano (MoU) unaripotiwa kuipa Ethiopia isiyo na bandari ufikiaji wa Bahari Nyekundu ili badala take Ethiopia kuitambua Somaliland kama nchi huru.
Somalia imetaja mpango huo kuwa ni kitendo cha "uchokozi" na kumrudisha nyumbani balozi wake mjini Addis Ababa.
Kuna ripoti kuwa balozi wa Ethiopia nchini Somalia pia amerejea Addis Ababa huku kukiwa na mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.