Waziri wa mambo ya nje wa china wang yi amejibu madai ya nato kuhusu beijing na urusi

Pia imeonya muungano wa nchi za Magharibi dhidi ya kuchochea makabiliano

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amejibu madai ya Nato "yasio na msingi" kwamba Beijing inaisaidia Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

Pia imeonya muungano wa nchi za Magharibi dhidi ya kuchochea makabiliano.

Bw Wang alitoa maoni yake kwa njia ya simu na mwenzake wa Uholanzi, saa chache baada ya viongozi wa nchi wanachama wa Nato kukusanyika Washington DC na kutoa tamko lililotaja vita.

Waliishutumu China kwa kuwa "mwezeshaji madhubuti" wa Urusi kupitia "uungaji mkono wake mkubwa upande wa viwanda vya ulinzi wa Urusi", katika baadhi ya matamshi yao makali kuhusu Beijing.

Waliitaka China kusitisha "msaada wote wa nyenzo na kisiasa" kwa juhudi za vita za Urusi kama vile usambazaji wa vifaa vya matumizi mara mbili, ambavyo vinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiraia na kijeshi.

Mataifa ya Magharibi awali yaliishutumu China kwa kuhamisha teknolojia ya ndege zisizo na rubani na makombora na picha za satelaiti hadi Urusi.

Marekani inakadiria takriban asilimia 70 ya zana za mashine na asilimia 90 ya vifaa vidogo vya elektroniki zinazoagizwa na Urusi sasa zinatoka China.

Beijing pia ilishutumiwa kwa kuendesha "shughuli mbaya za mtandao, ikiwa ni pamoja na taarifa potofu" kuhusu mataifa ya Nato.

Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi, Rais wa Marekani Joe Biden alisema kuwa alikuwa na majadiliano na viongozi wengine kuhusu kueleza madhara kwa China.

Share: