Waziri wa mambo ya nje wa china, afanya mikutano na viongozi wa marekani

Waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi, amewasili Washington Alhamisi kwa mkutano na maafisa waandamizi wa Marekani, kujadili masuala ya ushirikiano na kikanda kabla ya mkutano wa kilele unaoweza kufanyika baina ya viongozi wa nchi hizi mbili, mwezi ujao.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, ni mwenyeji wa waziri Wang katika dhifa ya kikazi katika wizara ya mambo ya nje baada ya mkutano mapema Alhamisi.

Mshauri wa usalama wa White House, Jake Sullivan, anafanya mazungumzo naye leo Ijumaa katika ukumbi wa Blair House, karibu na White House.

Muda mfupi tu kabla ya mkutano wake na waziri Blinken, wa saa mbili Alhamisi mchana, waziri Wang, aliwaeleza wanahabari kwamba China, na Marekani, zinapaswa kuwa na mazungumzo ya undani na mapana ili kupunguza hali ya kutoelewana, na kurejewa kwa maendeleo yenye nia njema, yaliyo thabiti, na endelevu

Share: