Waziri Bashe ameongeza kuwa Tanzania ina soko la kutosha kwa bidhaa za kilimo kutokana na idadi ya watu, mahitaji ya chakula na eneo la kuongeza thamani mazao.
Bashe amesema kuwa maeneo ya kilimo cha ngano, matunda na mbogamboga yana fursa kubwa sambamba na eneo la utengenezaji wa mafuta ya kupikia, mbolea, viuatilifu na uzalishaji wa mbegu bora za kilimo.
Mbali ya maeneo hayo Bashe pia amesema uzalishaji wa vifungashio ili kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno na eneo la kilimo cha umwagiliaji ni fursa kubwa zinazohitaji wawekezaji.
Waziri Bashe ameongeza kuwa Tanzania ina soko la kutosha kwa bidhaa za kilimo kutokana na idadi ya watu, mahitaji ya chakula na eneo la kuongeza thamani mazao.
Waziri Bashe ameyasema hayo leo katika mkutano na wawekezaji wa ndani ulioandaliwa na wizara ya kilimo na kuhudhuriwa na waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo.