Waziri wa afya azindua bodi mpya ya msd

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Juni 20, 2024 amezindua Bodi Mpya ya usimamizi wa kampuni tanzu ya MSD MEDPHARM Manufacturing ya Bohari kuu ya Dawa (MSD) pamoja na kampuni tanzu ya 'MSD Medipharm Manufacturing Company Ltd' itakayosimamia viwanda vya dawa na kusaidia upatikanaji wa huduma za Afya nchini.


Hafla hiyo imefanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa pia na Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daudi Msasi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Bi. Rosemarry Silaa, Mkurugenzi Mtendaji wa MSD na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mpya Bw. Mavere Tukai, Wajumbe wa bodi mpya pamoja na watumishi wa MSD.

Share: