Otárola alikuwa Waziri wa Ulinzi wa Peru hadi mwisho wa Mwaka 2022.
Waziri Mkuu, Alberto Otárola (57) amejiuzulu baada ya tuhuma za kuwa alijaribu kutumia Ushawishi wake kumsaidia Mwanamke mmoja kupata Mikataba ya Tenda Serikalini baada ya mazungumzo yake na Mwanamke huyo kuvuja
Kulingana na kipindi cha Panorama ambacho kilirusha Mazungumzo hayo, Mwanamke huyo Yaziré Pinedo (25) alipewa Mikataba Miwili kwa kazi katika Wizara ya Ulinzi mnamo Mwaka 2023 ambayo ilimuingizia jumla ya Dola za Marekani 14,000 (Takriban Tsh. Milioni 35.6)
Otárola alikuwa Waziri wa Ulinzi wa Peru hadi mwisho wa Mwaka 2022. Katika mazungumzo hayo Otárola anasikika akikiri mapenzi yake kwa Mwanamke huyo na kumwomba atume CV yake
Share: