Waziri mkuu wa israel benjamin netanyahu ameapa kuendeleza vita dhidi ya hamas

Hotuba ya Bw Netanyahu ilikatizwa na hekaheka za mara kwa mara kutoka kwa jamaa za mateka waliochukuliwa na Hamas wakati wa shambulio la Oktoba 7

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kuendeleza vita dhidi ya Hamas licha ya kukosolewa kimataifa kuhusu shambulizi la anga lililoua Wapalestina wengi mjini Rafah siku ya Jumapili.

Takriban watu 45 waliuawa, kwa mujibu wa wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas, huku mamia ya wengine wakipatiwa matibabu kutokana na majeraha ya moto.

Akizungumza katika bunge la Israel, Bw Netanyahu alisema shambulizi hilo lilikuwa "msiba mbaya" lakini akaongeza: "Sina nia ya kumaliza vita kabla ya kila lengo kufikiwa."

Alisema ni muhimu Israel kufanya "kila juhudi" kuwalinda raia na kusisitiza kuwa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linatumia "juhudi zao bora zaidi kutowadhuru wale wasiohusika" katika mzozo huo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litafanya mkutano wa dharura Jumanne, kwa ombi la Algeria, kujadili mgomo wa Rafah.

Katika taarifa yake siku ya Jumatatu, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema shambulizi hilp "limeua raia wengi wasio na hatia ambao walikuwa wakitafuta tu hifadhi kutokana na mzozo huu mbaya".

"Hakuna mahali salama Gaza. Hofu hii lazima ikomeshwe," alisema.

Hotuba ya Bw Netanyahu ilikatizwa na hekaheka za mara kwa mara kutoka kwa jamaa za mateka waliochukuliwa na Hamas wakati wa shambulio la Oktoba 7, ambao baadhi yao wamekuwa wakimkosoa kwa kushindwa kufanya makubaliano ya kurejeshwa kwa wapendwa wao.

"Huko Rafah tayari tumeahamisha takriban wakazi milioni moja wasio wapiganaji na licha ya jitihada zetu kubwa za kutowadhuru wasio wapiganaji, kwa bahati mbaya kitu kilienda vibaya,"

Share: