Henry aliingia makubaliano ya kupokea Askari wa Kulinda Amani, jambo lililoamsha vurugu zaidi kutoka kwa makundi ya Uhalifu
Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry amekubali kujiuzulu baada ya kuwepo Shinikikizo la Makundi ya Uhalifu yaliyomtaka kuachia madaraka kwa hiari kabla ya kurejea nchini humo kutoka Puerto Rico alikofikia wakati akirejea kutoka nchini Kenya.
Henry aliingia Madarakani baada ya Rais Jovenel Moise kuuawa ndani ya makazi yake Julai 7, 2021 na aliahidi kuirejesha nchi hiyo kwenye hali ya usalama kutoka katika vurugu zilizodumu kwa muda mrefu.
Katika ziara yake nchini Kenya, Henry aliingia makubaliano ya kupokea Askari wa Kulinda Amani, jambo lililoamsha vurugu zaidi kutoka kwa makundi ya Uhalifu ya Haiti, ambapo makundi hayo yalitoa Shinikizo la kumtaka ajiuzulu haraka.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kithure Kindiki amesema mpango wa kupeleka Askari 1,000 nchini Haiti uko katika hatua za mwisho.